TIKETI ZA ELEKTRONIKI ZIPO SOKONI
Mauzo
ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari
yameanza, hivyo wanatakiwa kununua mapema.
Mechi
hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers
kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kwa
washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya
Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao
mikononi, hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi
pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba
*150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa
*150*03.
Vilevile
tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa
tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo
wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.
YANGA YAINGIZA MIL 86/-, SIMBA MIL 53/-
Mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh.
139,850,000.
Yanga
iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake
liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba
ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza
sh. 53,815,00 kwa watazamaji 9,629.
Mgawanyo
kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
13,123,983.05, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu
ilipata sh. 20,650,211.50.
Uwanja
sh. 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh.
6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,450,025.09.
Mechi
ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu
ilipata sh. 12,595,211.50.
Uwanja
sh. 6,404,344.83, gharama za mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh.
3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,494,347.13.
Vilevile
tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo
katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo
watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.
0 comments:
Post a Comment