Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani jumanne ikiwa ni moja ya mashtaka ya uhalifu yanayomkabili kiongozi wa chama cha kiislamu.
Bwana Morsi na zaidi ya wanachama 100 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood wanakabiliwa na mashtaka kwa kutoroka jela mwaka 2011 na shutuma za kuua polisi wakati wa mapinduzi ambayo yamemuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Rais Hosni Mubarak na kumuingiza madarakani bwana Morsi.
Washtakiwa wengi wametambuliwa kuwa ni
wanachama wa kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas, kundi la
wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon na kikosi cha
Revolutionary Guard cha Iran.
Bwana Morsi na wanachama wengine
waandamizi wa kundi la Brotherhood pia wanakabiliwa na mashtaka kwa
shutuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji wa upizani wakati akiwa
madarakani.
Rais huyo wa zamani na watu wengine 35
pia watashtakiwa kwa shutuma za upelelezi kwa kushirikiana na kundi la
wapalestina la Hamas.
Jeshi la Misri lilimuondoa mamlakani
bwana Morsi mwezi July mwaka jana. Hosni Mubarak aliondolewa madarakani
kufuatia upinzani wa umma ambao ulianza Januari mwaka 2011.
Chanzo ni voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment