WIZARA ya kazi na ajira kupitia waziri wake Gaudentia Kabaka(pichani) amewataka
wakala wote wa
huduma za ajira
nchini kuwasilisha barua
za maombi za usajili wa
uwakala kwa kamishina
wa kazi .
Mwandishi wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com kutoka Dar ,Kenneth John anaripoti kuwa ,Tamko
hili limekuja baada
ya wizara hiyo,
kufanya utafiti na
kubaini kuwa utaratibu
wa kukodisha wafanyakazi,
unaofanywa na baadhi
ya wakala binafsi
wa huduma za
ajira ni kinyume
cha sheria za
huduma za ajira
Na 9 ya
mwaka 1999 (sura
243 kama ilivyorejewa
mwaka 2002)
Aidha
mheshimiwa Kabaka alisema
kuwa, kwa mujibu
wa kifungu 4
cha sheria hiyo ,majukumu ya
msingi ya wakala
wa huduma za
ajira, ni kuwaandaa
na kuwaunganisha watafuta
kazi na waajiri
kwa kutoa mafunzo
na ushauri elekezi
kwa watafuta kazi,kutafuta
fursa za ajira
na kutoa taarifa
za soko la
ajira, Hivyo mheshimiwa Kabaka
amesema kuwa mawakala
hawapaswi kuwa waajiri
wa wafanyakazi waliowatafutia kazi
kwa niaba ya
waajiri wengine.
Sambamba
na hayo mheshiwa
Kabaka alisema kuwa
uchunguzi walioufanya ulibaini
kwamba, utaratibu huu
ni ujanja unaotumiwa
na baadhi ya
waajiri, pamoja na
mawakala kwa
lengo la kukwepa
kodi na kujipatia
faida kwa njia
ya kutotoa haki
za msingi za
wafanyakazi kwa mujibu
wa sheria za
kazi.Mheshimiwa Kabaka aliendelea
kusema kuwa baadhi
ya makampuni yanayokodisha
wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki
na TRA na
kubainika kukwepa kodi
ya mapato ya
ajira (PAYE) na
kodi ya mapato
ya kampuni kinyume
na kifungu cha
7 cha sheria
ya kodi ya
mapato ya mwaka
2004 (sura 332
kama ilivyorejewa mwaka
2008)
Pamoja
na hayo mheshiwa
Kabaka alisema kuwa,
pia uchunguzi ulibaini
athari mbalimbali kwa
wafanyakazi wanaoajiriwa kwa
utaratibu wa huduma
hizo za mawakala,
ikiwa ni pamoja
na wafanyakazi kukosa
haki ya hifadhi ya
jamii kama vile
likizo ya uzazi
na matibabu ambapo
ni kinyume na
sheria mbalimbali za
mifuko ya hifadhi
ya jamii,Uwepo wa
ubaguzi katika malipo
ya mishahara kwa
kazi ya aina
moja ,kukosa fursa ya
kujiendeleza kielimu na
mafunzo,kukosekana kwa usalama
na uhakika wa
ajira pamoja na
wafanyakazi kulipwa mishahara
ya kima cha
chini kinyume na
sekta wanayofanyia kazi.
Vile
vile kutokana na
hayo yote wizara
imeamua kusitisha mara
moja utaratibu wa
mawakala kuwaajiri wafanyakazi , wanaowatafutia kazi.
Aidha , mawakala na
kampuni husika waliopo
katika utaratibu huo
kwa sasa wanapaswa
kuwahamisha wafanyakazi waliokodishwa
kutoka kwa wakala
kwenda kwa kampuni
husika .
Hivyo waziri Kabaka
amewaagiza waajiri na
mawakala kukamilisha zoezi
hilo ndani ya
kipindi cha mwezi
mmoja na kuhakikisha
wanawasilisha taarifa za
utekelezaji kwa katibu
mkuu wizara ya
kazi na ajira
kabla au ifiakapo
February 28, 2014
Halikadharika waziri Kabaka ameelekeza wakala wa huduma za ajira nchini , kuwa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya usajili wa uwakala kwa kamishina wa kazi ,ili waweze kufanya shughuli za uwakala wa huduma za ajira kisheria, na maombi hayo ameagiza yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili.Kabaka aliendelea kusema kuwa baada ya muda huo, wakala ambaye hatokuwa na kibali cha kamishina wa kazi hataruhusiwa kuendesha shughuli za huduma za ajira nchini. Na kwa wale mawakala watakaopata leseni ya kamishina wa kazi , watatangazwa ili watambulike na umma.
0 comments:
Post a Comment