Friday, 31 January 2014

UHAMISHO SIKU YA MWISHO: ZOUMA CHELSEA, MAN CITY NA WAWILI WA PORTO, ARSENAL YAKOSA?

>>YOBO ARUDI ENGLAND!!
TONI_KROOS2USIKU huu wa Leo, Saa 8 na Nusu, Dirisha la Uhamisho, litabamizwa na kufungwa hadi Juni na hii imeamsha patashika ya Dakika za mwsiho za Usajili wa Wachezaji.
PATA HABARI MOTO KWA UFUPI:
CHELSEA YAKARIBIA KUMSAINI KURT ZOUMA TOKA ST ETIENNE
Chelsea ipo karibu kumsaini Kurt Zouma wa St Etienne ya France.
Beki huyo mwenye Miaka 19 anatarajiwa kusainiwa na Chelsea hii Leo na kubakishwa Klabu hiyo ya France kwa Mkopo.
Chelsea tayari imewasaini Nemanja Matic na Mohamed Salah kwenye Dirisha hili la Uhamisho.
MAN CITY YAWATAKA WAWILI WA PORTO
Manchester City wapo hatua nzuri ya kuwanasa Wachezaji wawili wa FC Porto, Eliaquim Mangala na Fernando.
Beki wa France, Mangala, Miaka 22, anathaminiwa Pauni Milioni 35 wakati Fernando, Raia wa Brazil mwenye Miaka 26, yupo chini ya hapo.
Ikiwa Wachezaji hao watatua Etihad, basi njia itakuwa nyeupe kwa Joleon Lescott kwenda West Ham United.
ARSENAL YAELEKEA KUWAKOSA JULIAN DRAXLER NA MIRKO VUCINIC!
Kwa mujibu wa Magazeti makubwa huko Uingereza, Arsenal imekwama kuwasaini Julian Draxler wa Schalke na Mirko Vucinic wa Juventus na sasa inahaha kuwasaini kwa Mkopo Alvaro Morata wa Real Madrid na Christian Tello wa Barcelona kitu kinachodhaniwa ni kigumu.
YOBO ATUA NORWICH
Norwich imemsaini Beki Veterani wa Nigeria, Joseph Yobo, kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu kutoka Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Habari hizi zimethibitishwa na Meneja wa Norwich, Chris Houghton, ambae amelazimika kusaka Mtu kuziba nafasi ya Majeruhi Michael Turner.
Yobo, mwenye Miaka 33, alijiunga na Fenerbahce Mwaka 2010 akitokea Everton kwa Mkopo ambao baadae ulikuwa Uhamisho wa kudumu baada ya kuitumikia Everton tangu 2002.

0 comments: