>>AGUSIA MECHI YA ETHAD NA CITY JUMATATU IJAYO!
KWA mujibu wa Meneja wao, Chelsea
watakuwa wamekamilika Msimu ujao kwa kutwaa Ubingwa lakini Msimu huu
watazisukuma Arsenal na Manchester City hadi mwishoni kwenye mbio za
Ubingwa kama ilivyodokezwa hii leo na Jose Mourinho.
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO=Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
22 |
24 |
51 |
2 |
Man City |
22 |
38 |
50 |
3 |
Chelsea |
22 |
23 |
49 |
4 |
Liverpool |
22 |
25 |
43 |
5 |
Tottenham |
22 |
3 |
43 |
6 |
Everton |
22 |
15 |
42 |
7 |
Man United |
22 |
9 |
37 |
Jumatano Usiku, Chelsea itakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na West Ham kwenye Mechi ya Ligi huku wakiwa Nafasi ya 3, Pointi 1 nyuma ya Man City walio Nafasi ya Pili na 2 nyuma ya Vinara Arsenal.
Lakini, Leo hii akiongea na Wanahabari
ambao waligawiwa Mvinyo kusherehekea Miaka yake 51 ya Kuzaliwa, kwenye
Mahojiano maalum kwa ajili ya Mechi yao ya Kesho na West Ham, Mourinho
alitamka: “Nafasi ya kunywa Shampeni hapo baadae ni nzuri lakini si
Msimu huu”
Mourinho alifafanua kuwa lengo lao ni
kujenga Timu imara kwa ajili ya Msimu ujao na tayari ameshamuuza Kiungo
wa SpainJuan Mata kwa Man United na kumnunua Kijana wa Misri Mohamed
Salah kutoka Klabu ya Uswisi, Basle ambae anaungana na mpya mwingine
Kiungo Nemanja Matic kutoka Benfica.
Akigusia Mechi kubwa ya Jumatatu ijayo
ya Ligi ambayo watasafiri kwenda huko Etihad kucheza na Man City,
Mourinho alisema: “Tunataka kucheza na City tukiwa tuna ushindani na sio
kuwa nyuma Pointi 10.”
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jan 29: Chelsea V West Ham [Ligi]
Feb 3: Man City V Chelsea [Ligi]
Feb 8: Chelsea V Newcastle [Ligi]
Feb 11: West Brom V Chelsea [Ligi]
Feb 15: Man City V Chelsea [FA CUP]
Feb 22: Chelsea V Everton [Ligi]
Feb 26: Galatasaray V Chelsea [UCL]
Akiigusia Mechi yao na West Ham,
Mourinho alikiri itakuwa ni Mechi ngumu kwao na pia watamkosa Straika
wao Fernando Torres ambae ameumia lakini Mourinho ameonyesha imani yake
kubwa kwa Samuel Eto'o hasa baada kupiga Hetitriki walipoichapa Man
United Bao 3-1 Jumapili iliyopita Uwanjani Stamford Bridge.
0 comments:
Post a Comment