"UN umeomba vile vikosi vya jeshi letu
vilivyopo kule Sudan Kaskazini vigawanywe, ili nusu viende Juba ambako
kwa sasa kuna matatizo zaidi na vitakavyosalia vibaki Darfur.
"Hivyo hilo ni suala ambalo Waziri Membe amelifikisha mezani kwa Rais Kikwete, tunachosubiria ni majibu yake ili waanze kujiandaa na kupanga 'logistics' vizuri," alisema.
Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alinukuliwa na Shirika la Habari la Uingereza Idhaa ya Kiswahili (BBC), akisema kwamba Umoja wa Mataifa (UN), wameiomba Tanzania kupeleka wanajeshi Sudan Kusini ili kwenda kurejesha amani.
Membe alisema kuwa wamepokea maombi hayo ya UN wiki hii na kwamba Rais Jakaya Kikwete na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini wanashauriana na makamanda wao wa majeshi, ili kuangalia uwezekano wa kutekeleza ombi hilo la UN.
Membe alisema hatua hiyo ya UN imekuja baada ya kuutambua uwezo na mchango mkubwa wa Tanzania katika kulinda amani kwenye nchi za Lebanon, Darfur na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
"Umoja wa Mataifa unautambua uwezo wa vikosi vyetu vya jeshi na ndio maana wameona ipo haja ya kuwatumia vijana wetu kwenda kurejesha amani Sudan Kusini, Rais Kikwete na mwenzake wa Afrika Kusini wanajadiliana pamoja na makamanda wao kuangalia uwezekano," alisema Membe.
Membe alisema kuwa maombi hayo ya UN pia yalipelekwa kwa Serikali ya Afrika Kusini.
Sudan Kusini imekuwa kwenye machafuko, kutokana na kutofautiana kwa Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake, Dk. Riek Machar, ambaye ameingia msituni kutaka kumpindua kiongozi wake.
Mapigano hayo yamesababisha idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo kuyakimbia makazi yao, huku wengine wakipoteza maisha.
Vikosi vya Jeshi la Tanzania vilivyopo Darfur vimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na waasi, hali inayoufanya Umoja wa Mataifa kuwataka wapiganaji hao wa JWTZ kwenda Juba kulinda amani. Chanzo: mtanzaniaa

0 comments:
Post a Comment