Na Martha Magessa
Wanawake
wameshauriwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia siasa au
serikali za mitaa bila kusubiri nafasi za kuteuliwa.
Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa
Lediana Mng'ong'o amesema, wanawake wadumishe umoja na kutumia fursa za
kugombea nafasi za uongozi ili kuweza kuzikomboa jamii kwani mwanamke ni
nguzo ya taifa.
Mbunge huyo wa viti maalum, amesema
hayo katika kikao cha umoja wa wanawake wa Iringa vijijini kupitia chama
cha mapinduzi ambapo wamekuwa na umoja wao ambao umekuwa ukisaidia
kudumisha amani nchini.
Ameongeza kuwa, licha ya kudumisha
umoja wanawake wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa elimu juu ya
maambukizi ya virusi vya ukimwi na kupinga unyanyasaji wa kijinsia.
Aidha wanawake hao, wameeleza faida za kujiunga na kikundi cha umoja hao kwani wameweza kusomesha familia zao.
Katika kikao hicho mbunge huyo wa viti
maalumu amechangia kikundi hicho cha wanawake shilingi laki tano
kwaajili ya kuwaongezea miradi mbalimbali wanawake hao.
Hata hivyo, mwenyekiti wa UWT Wilaya
ya Iringa vijijini kwa niaba ya kikundi cha wanawake hao amesema,
wataendeleza umoja huo ili kuweza kulinda taifa na kupingana na
wanasiasa wasiotekeleza majukumu yao katika jami
0 comments:
Post a Comment