>>LEO SPURS v MAN CITY, CHELSEA v WEST HAM!
LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumanne Januari 28
Man United 2 Cardiff 0
Norwich 0 Newcastle 0
Southampton 2 Arsenal 2
Swansea 2 Fulham 0
Crystal Palace 1 Hull 0
Liverpool 4 Everton 0
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge alifunga mabao mawili huku akikosa mkwaju wa penati lakini nahodha Steven Gerrard alikuwa nyota wa mchezo kwenye mechi ya 222 baina ya mahasimu hawa wa kitongoji cha Merseyside,kwenye mchezo Gerrard na Luis Suarez walifunga bao moja moja na kuiongoza Liverpool kuifunga Everton mabao 4-0.
Arsenal ilishindwa kujikita kileleni baada ya kulazimishwa
sare ya mabao 2-2 na Southampton ugenini kwenye uwanja wa St Mary’s.
Mchezaji ghali kwenye historia ya klabu ya Man Utd Juan Mata alivaa jezi yake namba 8 ya Man Utd kwa kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cardiff City.
Kwenye mchezo huo mabao ya Man U yalifungwa na Robin Van Persie pamoja na Ashley Young.
RATIBA YA MECHI ZA LEO
MAN UNITED 2 CARDIFF 0
Mchezaji mpya, Juan Mata, alianza Mechi
yake ya kwanza kwa Man United na kuanzisha muvu iliyozaa Bao la kwanza
Mfungaji akiwa Robin van Persie aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza
tangu Desemba 1o alipoumia.
Bao la Pili lilifungwa vizuri sana na
Ashley Young na kuipa Man United ushindi wa Bao 2-0 dhidi ya Cardiff
City ambayo Meneja wao mpya, Ole Gunnar Solksjaer, Nguli wa Man united,
alipokewa vizuri na Mashabiki wa Old Trafford.
SOUTHAMPTON 2 ARSENAL 2
Vinara wa Ligi, Arsenal, walinasa
kuendelea kupaa juu kileleni baada ya kutoka Sare ya Bao 2-2 na
Southampton ambao ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 21 kwa Bao
la Jose Fonte lililodumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Olivier Giroud aliisawazishia Arsenal katika Dakika ya 48 na Cazorla kupiga Bao la Pili kwa Arsenal.
Adam Lalallan aliipa Southampton Bao la
kusawazisha katika Dakika ya 54 na Mechi kwisha 2-2 na Arsenal kumaliza
Mtu 10 bbada Kiungo wao Mathieu Flamini kulambwa Kadi Nyekundu Dakika ya
80 kwa rafu mbaya.
SWANSEA 2 FULHAM 0
Bao za Jonjo Shelvey na Chico zimewapa ushindi wa Bao 2-0 walipoibamiza Fulham.
CRYSTAL PALACE 1 HULL CITY 0
Crystal Palace wameifunga Hull City Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 16 la Puncheon.
LIVERPOOL 4 EVERTON 0
Dabi ya Merseyside imemalizika kwa Liverpool kuwaumbua Watani zao Everton Uwanjani Anfield na kuwatandika Bao 4-0.
Hadi Mapumziko, Liverpool walikuwa mbele 3-0 kwa Mabao ya Gerrard, Sturridge, Bao 2, na Suarez kupiga la 4 Kipindi cha Pili.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 23 | 24 | 52 |
2 | Man City | 22 | 38 | 50 |
3 | Chelsea | 22 | 23 | 49 |
4 | Liverpool | 23 | 29 | 46 |
5 | Tottenham | 22 | 3 | 43 |
6 | Everton | 23 | 11 | 42 |
7 | Man Utd | 23 | 11 | 40 |
8 | Newcastle | 23 | 4 | 37 |
9 | Spton | 23 | 4 | 32 |
10 | Swansea | 23 | -4 | 24 |
11 | Aston Villa | 22 | -7 | 24 |
12 | Norwich | 23 | -17 | 24 |
13 | Hull | 23 | -7 | 23 |
14 | Crystal | 23 | -16 | 23 |
15 | West Brom | 22 | -5 | 22 |
16 | Stoke | 22 | -14 | 22 |
17 | Fulham | 23 | -28 | 19 |
18 | West Ham | 22 | -11 | 18 |
19 | Sunderland | 22 | -15 | 18 |
20 | Cardiff | 23 | -23 | 18 |
0 comments:
Post a Comment