Kama
mfatiliaji wa muziki wa Dansi Tanzania,jina la Mc D si jina geni
kwako,jina lake halisi ni Masoud Mohamed,ni mpiga tumba kutoka bendi ya
African Stars Band’Twanga pepeta’ taarifa hizi zimetangazwa usiku huu na
kuthibitishwa na msemaji wa Twanga pepeta Hassan Rehani .
Taarifa zaidi inasema kuwa Mc D alikua yukoMoshi kwa ajili ya
matibabu zaidi ya miezi miwili na hali yake iliendelea vizuri hadi usiku
huu wa January 27 hali yake ilipobadilika na kufariki dunia.
Wiki chache nyuma ilisemekana Mc D alikua akiendelea vizuri kwani
hatua ngumu ya dozi ya kali ya kifua kikuuu alikua kashaivuka na sasa
alikua amebadilishiwa dawa,aliongea kwa matumaini makubwa kuwa atarejea
jukwaani muda si mrefu.
Miongoni mwa bendi alizozitumikia Mcd enzi ya uhai wake ni pamoja na Diamond Sound,Mashujaa Band na Twanga pepeta.
0 comments:
Post a Comment