Monday, 27 January 2014

UPANUZI WA BARABARA MKOANI MOROGORO BADO MAJANGA TU

 
ujenzi a08c1
Kinyume na matarajio ya wengi, mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Morogoro, kilomita 21 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi Kimara umekuwa kero kubwa kwa wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri kupitia katika barabara hiyo. Tangu kuanza kwa mradi huo yapata miaka miwili hivi iliyopita, tumeshuhudia wananchi wengi wanaotumia barabara hiyo wakionyesha kuchoshwa na adha wanazozipata kutokana na misururu mirefu ya magari barabarani. Gari haziendi mbele wala kurudi nyuma, ni kero kubwa.

0 comments: