RPC Mungi
Watu
wanne{4} wamefariki dunia katika matukio manne tofauti mkoani Iringa
akiwemo mtoto wa mwaka mmoja na nusu kufa baada ya kutumbukia katika
ndoo ya maji.
Mwandishi wetu kutoka Iringa Diana Bisangao anahabarisha kuwa akizungumza na mtandao huu ofisini
kwake leo, kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 29 januari
majira ya saa 9:00 kamili mchana maeneo ya Ugele kata ya mtwivila
manipaa ya Iringa .
Alimtaja
mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Neema Lukosi na kusema kuwa alikuwa
anacheza karibu na ndoo yenye maji hadi kufikia hatua ya kuingia kwenye
ndoo hiyo ambapo maji yalimzidi nguvu hadi kufa papohapo.
Mungi
alisema kuwa chanzo kifo cha mtoto huyo ni uzembe wa mzazi wake
kushidwa kumwangalia hivyo kuwataka wazazi au walezi kuwa makini na
watoto wao ili kuwaepushia mambo ya hatari.
Katika
tukio linguine huko katika maeneo ya Kata ya Malenga Makali tarafa ya
Ismani Iringa vijijini , Hilda Mzena (36) ambaye ni mkulima alifariki
dunia baada ya kuuliwa na mtu mmoja jina John Mgoni kwa kukatwa na kitu
chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake huku chanzo kikiwa ni
wivu wa kimapenzi na mtuhumiwa anatafutwa na polisi.
Wakati
huohuo huko maeneo ya Kijiji cha Igunga kata ya Ilula wilaya ya Kilolo
mtu anaejulikana kwa jina la Hamis Govela (57) alifariki dunia baada ya
kujinyonga kwa kutumia kamba ya koti lake.
Na tukio lingine Erasto Ilomo (35) alifariki dunia baada ya kuanguka njiani akiwa anatembea
Kamanda
Mungi alisema kuwa Tukio hilo lilitokea maeneo ya magari mabovu kata ya
kitanzini manispaa ya Iringa na kuongeza kuwa mtu huyo alidondoka
ghafla na kufa hapohapo na jeshi lapolisi linaendelea na uchunguzi ili
kufahamu chanzo cha kifo chake.
0 comments:
Post a Comment