Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera.
Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na
shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann
alikuwa na umri wa miaka 39.
Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema :
"Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda
watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.''
Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi
mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann
kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa
mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza
mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa
Ethiopia,'' alisema Solomon
Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye
pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama
mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.
'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye
kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya.
Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.'' alisema Elizabeth Blunt
aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua
usukani kutoka kwake.
"Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC
nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu
Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC
Nairobi Kenya.
Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London
Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu
wakati huu mgumu.
0 comments:
Post a Comment