Wednesday, 29 January 2014

SHULE ILIYOPO ENEO LENYE MGODI MKUBWA WA DHAHABU YAFUGWA KWA KUKOSA CHOO.

........................



Mwonekano  wa mgodi  huo BULYANHULU Kahama
.....................................................................................

MWANDISHI ,WILIAM BUNDALA WA   ,KAHAMA 

IDARA ya Ukaguzi wa Shule za Msingi wilayani Kahama imeifunga Shule ya Msingi ya Bugarama eneo uliopo Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick gold Mines baada ya kukosa vyoo.
Mkaguzi mkuu wa Shule za Msingi wilayani Kahama;Ephraimu Kaijuko amesema shule hiyo waliifunga jana baada ya kubaini wanafunzi 1500 wanaosoma hapo hawana pa kujisaidia na badala yake hujisaidia vichakani.

Kaijuko amesema hali hiyo ni hatari katika afya za watoto hao ili kuwanusuru na maradhi ya kuambukizwa idara yake imeifunga shule hiyo mpaka pale ujenzi wa vyoo utakapokamilika.

Amesema Idara yake sasa inazunguka wilaya nzima kufanya ukaguzi wa mapungufu mbali mbali yaliyomo kwenye shule za msingi huku kubwa zaidi likiwa ni vyoo.

Wilayani Kahama idadi kubwa ya shule za msingi hazina vyoo baada ya vilivyokuwepo baada ya kujengwa mwaka 2002 kupitia mpango wa MMEM kubomoka na vingine kuchakaa baada ya kujengwa chini ya kiwango.

0 comments: