Monday, 27 January 2014

CHADEMA WAANZA KAMPENI ZA URAISI KUELEKEA UCHAKUZI WA MWAKA 2015

Willibrod-Slaa 9cd30

Viongozi mbalimbali wa Chadema wameanza kupiga kampeni za urais mwaka 2015 kupitia Operesheni Pamoja Daima. 
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Njombe huku mvua kubwa ikinyesha jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa, atawashtaki na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka 2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha masilahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za Serikali watapata wakati mgumu.
"Tutakuwa wakali kwa walarushwa," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema watendaji walarushwa na wezi watashtakiwa ili mali walizowaibia Watanzania zirejeshwa Serikalini.
"Ninawapa miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu, vigogo hao kurudisha mali walizoiba vinginevyo watajuta kwa sababu tutawashtaki tutakapoingia madarakani." alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema chama hicho kitatumia kila aina ya 'silaha' kilichonayo kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama hicho 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ndesamburo alisema hakuna kikwazo kuyatwaa majimbo hayo kwa vile CCM, kimeshindwa kuwaletea Watanzania maisha bora kama waliyojinadi mwaka 2010.
Kwa sasa Chadema kinashikilia majimbo ya Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo (2000-2015), Jimbo la Hai na Jimbo la Rombo wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishikilia majimbo matano.
CCM kinashikilia majimbo ya Moshi Vijijini, Siha, Mwanga, Same Mashariki na Magharibi wakati Tanzania Labour Party (TLP), kikishikilia Jimbo la Vunjo kupitia Mbunge wake, Augustine Mrema.
Akizungumza mjini Singida jana, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu aliwataka Watanzania kumchagua rais mwadilifu siyo anayehonga hata mapadri fedha chafu zilizotokana na ufisadi.
Alisema baadhi ya viongozi (bila kuwataja) hivi sasa wanapita kwenye nyumba za ibada kutoa rushwa na kudai kwamba zamu yao ya kuwa rais imewadia. Chanzo: mwananchi

0 comments: