Thursday, 30 January 2014

JOSE MOURINHO: ‘WEST HAM INA STAILI YA KARNE YA 19!’

>>JOSE AKASIRISHWA KUGANGAMALA KWA WEST HAM!!  

>>BIG SAM: “HAKUBALI, TUMEMSHINDA MBINU!!”!

JOSE_MOURINHO-poaJose Mourinho ameishutumu West Ham kwa kucheza ‘Soka la Karne ya 19’ baada ya kuibana Chelsea Jana Usiku huko Stamford Bridge na kutoka Sare ya 0-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na kuwabakisha Nafasi ya 3.BIG_SAM
Chelsea walikuwa na Mashuti 39 Golini na West Ham, waliojihami muda mwingi wa Mchezo, wakiwa na Shuti 1 tu.
Jose Mourinho, akikerwa baada ya Mechi, alisema: “Hii si Ligi bora, hili ni Soka la Karne ya 19!”
Aliongeza: “Kitu pekee ningeweza kufanya ni kuja na Msumeno wa ‘Black and Decker’ kupasua Ukuta!”
Ingawa Chelsea walikuwa na Mashuti mengi Golini, lakini ni 9 tu yalilenga Goli na Kipa wa West Ham, Adrian, aliokoa Mipira mitatu tu toka kwa John Terry, Samuel
Eto'o na Frank Lampard huku Oscar na Demba Ba, alietokea Benchi, wakizuiwa na Posti.

DONDOO MUHIMU:
-West Ham wamemudu kutofungwa Bao katika Mechi 10 za Ligi wakiungana na Arsenal kwa Rekodi hiyo!

Jaribio pekee la West Ham Golini lilikuwa Kichwa cha James Tomkins kuokolewa na Kipa Petr Cech..
Mourinho alizidi kulalamika: “Ni ngumu kucheza Soka wakati Ni Timu moja tu inayotaka kucheza!”
Lakini Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, ambae Timu yake bado ni moja ya Timu 3 za Mkiani, alijibu: “Hakubali, hawezi? Hakubali kwa sababu tumemshinda mbinu- hawezi kumudu! Mwache aseme lolote sisi hatujali! Napenda kuwaona Wachezaji wa Chelsea wakilia kwa Refa, wakijaribu kumtisha, Jose akirukaruka pembeni na kusema tunacheza Soka bovu!”
Big Sam, kama anavyoitwa Sam Allardyce, alibainisha kuwa mbinu yao kubwa ilikuwa ni kwenye Sehemu mbili, ya kwanza ikiwa ni kuwazuia Hazard, Oscar, Willian na Eto'o kufunga na nyingine ni kuwabana Chelsea wasifunge kwenye ‘Mipira iliyokufa.’
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
F
GD
PTS
1
Man City
23
17
2
4
68
26
42
53
2
Arsenal
23
16
4
3
45
21
24
52
3
Chelsea
23
15
5
3
43
20
23
50
4
Liverpool
23
14
4
5
57
28
29
46
5
Tottenham
23
13
4
6
30
31
-1
43
6
Everton
23
11
9
3
35
24
11
42
7
Man United
23
12
4
7
38
27
11
40
8
Newcastle
23
11
4
8
32
28
4
37
9
Southampton
23
8
8
7
31
27
4
32
10
Aston Villa
23
7
6
10
26
32
-6
27
11
Swansea
23
6
6
11
29
33
-4
24
12
Norwich
23
6
6
11
18
35
-17
24
13
Hull
23
6
5
12
22
29
-7
23
14
Crystal Palace
23
7
2
14
15
31
-16
23
15
West Brom
23
4
10
9
27
33
-6
22
16
Stoke
23
5
7
11
22
37
-15
22
17
Sunderland
23
5
6
12
22
36
-14
21
18
West Ham
23
4
7
12
22
33
-11
19
19
Fulham
23
6
1
16
22
50
-28
19
20
Cardiff
23
4
6
13
17
40
-23
18
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 1
15: 45 Newcastle v Sunderland
15: 45 West Ham v Swansea
18:00 Cardiff v Norwich
18:00 Everton v Aston Villa
18:00 Fulham v Southampton
18:00 Hull v Tottenham
18:00 Stoke v Man Utd
Jumapili Februari 2
16:30 West Brom v Liverpool
19:00 Arsenal v Crystal Palace
Jumatatu Februari 3
23:00 Man City v Chelsea

0 comments: