FEBRUARI ITATOA NANI MBIVU, NANI MBICHI!
>>LIVERPOOL, MAN UNITED 5!!
>>NDANI ZIMO: LIVERPOOL v ARSENAL X2, CITY v CHELSEA X2, ARSENAL v MAN UNITED!
WACHAMBUZI wa Soka wamedai Mwezi
Februari ndio utapambanua nani ataelekea kwenye Mafanikio kwa Msimu huu
wa 2013/14 kwenye kutwaa Ubingwa wa England, FA CUP na UEFA CHAMPIONZ
LIGI.
Zile Timu 4 za juu kwenye Msimamo wa
Ligi Kuu England, Vinara Arsenal, Manchester City, Chelsea na Liverpool,
zinachuana vikali kwenye mbio za Ubingwa huku Mabingwa Watetezi
Manchester United wakijikongoja toka Nafasi ya 7.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 23 | 24 | 52 |
2 | Man City | 22 | 38 | 50 |
3 | Chelsea | 22 | 23 | 49 |
4 | Liverpool | 23 | 29 | 46 |
5 | Tottenham | 22 | 3 | 43 |
6 | Everton | 23 | 11 | 42 |
7 | Man Utd | 23 | 11 | 40 |
Wakati
Arsenal, City na Chelsea zipo pia kwenye vinyang’anyiro vya FA CUP na
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Liverpool wao wapo kwenye FA CUP tu na
watapambana na Arsenal Wikiendi ya Februari 15.
Kwa Timu hizo 4 za juu kwenye Ligi,
Arsenal ndio inaonekana kuwa na Ratiba ngumu kwani Mwezi Februari
itacheza na Liverpool, kisha Man United na tena na Liverpool, ndani ya
Wiki, na kufuatia na Mechi ngumu dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Bayern
Munich, kwenye UCL.
Kwenye Kipindi hicho, Mechi ngumu kwa Chelsea ni ile mitanange miwili dhidi ya Man City kwenye Ligi na FA CUP.
Kwa Liverpool wao watacheza mara mbili na Arsenal kwenye Ligi na FA CUP.
Man City, licha ya kukutana mara mbili
na Chelsea, pia wataivaa Barcelona kwenye UCL na tena hii itakuwa Siku 3
tu baada ya kupambana na Chelsea kwenye FA CUP.
Kwa Mabingwa Man United, kimtazamo, Mechi ngumu pekee kwao ni ile ya Emirates ya Ligi dhidi ya Arsenal.
RATIBA:
**Mechi zote ni Ligi Kuu England isipokuwa inapotajwa
ARSENAL
2 FEB: Arsenal v Crystal Palace
8 FEB: Liverpool v Arsenal
12 FEB: Arsenal v Man Utd
15 FEB: Arsenal v Liverpool [FA CUP]
19 FEB: Arsenal v Bayern Munich [UCL]
22 FEB: Arsenal v Sunderland
CHELSEA
3 FEB: Man City v Chelsea
8 FEB: Chelsea v Newcastle
11 FEB: West Brom v Chelsea
15 FEB: Man City v Chelsea [FA CUP]
22 FEB: Chelsea v Everton
26 FEB: Galatasaray v Chelsea [UCL]
LIVERPOOL
2 FEB: West Brom v Liverpool
8 FEB: Liverpool v Arsenal
12 FEB: Fulham v Liverpool
15 FEB: Arsenal v Liverpool [FA CUP]
23 FEB: Liverpool v Swansea
MAN CITY
3 FEB: Man City v Chelsea
8 FEB: Norwich v Man City
12 FEB: Man City v Sunderland
15 FEB: Man City v Chelsea [FA CUP]
18 FEB: Man City v Barcelona [UCL]
22 FEB: Man City v Stoke
MAN UNITED
1 FEB: Stoke v Man Utd
9 FEB: Man Utd v Fulham
12 FEB: Arsenal v Man Utd
22 FEB: Crystal Palace v Man Utd
25 FEB: Olympiakos v Man Utd [UCL]
0 comments:
Post a Comment