STRAIKA wa Cardiff City anaetoka Nigeria, Peter Odemwingie, amejiunga na Stoke City kwa kubadilishana na Kenwyne Jones, anaetoka Trinidad and Tobago, ambae ameenda Cardiff lakini habari moto zaidi ni ule uwezekano mkubwa wa Kiungo wa Germany Toni Kroos kutua Old Trafford.
SOMA ZAIDI:
PETER ODEMWINGIE AJIUNGA STOKE, KENWYNE JONES ASAINI CARDIFF!
STRAIKA
wa Cardiff City anaetoka Nigeria, Peter Odemwingie, amejiunga na Stoke
City kwa kubadilishana na Kenwyne Jones, anaetoka Trinidad and Tobago,
ambae ameenda Cardiff.
Odemwingie, Miaka 32, amekuwa hajatulia
na Cardiff tangu ajiunge nayo mwanzoni mwa Msimu na tangu aje Meneja
mpya Ole Gunnar Solskjaer amekuwa hapati namba.
Nae Jones, Miaka 29, amekuwa na mzozo na
Stoke City tangu agome kucheza Mechi na Liverpool kitu kilichomfanya
Meneja Mark Hughes amtupe nje.
Wakati Odemwingie amesaini Mkataba wa Miezi 18 na Stoke, ule wa Jones na Cardiff haukutangazwa.
Odemwingie, ambae amefunga Bao 2 katika
Mechi 17 na Cardiff atangu ahamie kutoka West Brom kwa Dau la Pauni
Milioni 2, anaweza kucheza Mechi ya Jumatano ya Ligi dhidi ya Sunderland
huko Stadium of Light.
Jones alijiunga na Stoke Agosti 2010 akitoka Sunderland kwa Dau la Pauni Milioni 8 na kuifungia Bao 26 katika Mechi 115.
0 comments:
Post a Comment