>>JUMATANO: BILBAO v ATLETICO, BARCA v LEVANTE!
REAL
MADRID, wakicheza kwao Santiago Bernabeu, katika Mechi ya Marudiano ya
Robo Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, wameifunga
Espanyol Bao 1-0 na kuibwaga nje.
Real waliifunga Espanyol Bao 1-0 katika
Mechi ya kwanza iliyochezwa Jiji la Barcelona Wiki iliyopita na hivyo
kutinga Nusu Fainali kwa Jumla ya Bao 2-0.
Bao za Real Madrid zilifungwa na Jese Rodriguez katika Dakika ya 7.
Espanyol walimaliza Mechi Mtu 10 baada
ya Mchezaji wao, Victor Sanchez Mata, kupewa Kadi Nyekundu Dakika ya 76
baada Kadi za Njano mbili.
Kwenye Nusu Fainali Real watacheza na
Mshindi wa Mechi ya Jumatano kati ya Athletic de Bilbao na Atletico
Madrid, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey, huku Atletico
wakiwa mbele kwa Bao 1-0 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza.
Mechi nyingine ya Jumatano ni huko Nou Camp, Barcelona watakaporudiana na Levante ambayo ilichapwa Nyumbani kwao Bao 4-1.
Mechi ya mwisho ya Marudiano ya Robo
Fainali ni Alhamisi kati ya Real Racing Santander na Real Sociedad ambao
wako mbele kwa Bao 3-1.
VIKOSI VILIVYOANZA:
REAL MADRID: Casillas; Arbeloa, Sergio Ramos, Nacho, Coentrao; Xabi Alonso, Illarramendi; Di Maria, Isco, Cristiano Ronaldo; Jese.
ESPANYOL: Kiko Casilla;
Raul Rodriguez, Sidnei, Hector Moreno, Capdevila; Victor Sanchez, Alex
Fernandez, Abraham; Torje, Pizzi, Sergio Garcia.
COPA del REY
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI:
[Saa za Bongo]
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Jumla ya Magoli Mechi 2]
Jumanne Januari 28
Real Madrid 1 RCD Espanyol 0 [2-0]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano Januari 29
22:00 Athletic de Bilbao v Atlético de Madrid [0-1]
24:00 FC Barcelona v Levante [4-1]
Alhamisi Januari 30
23:00 Real Racing Santander v Real Sociedad [1-3]
NUSU FAINALI
Mechi ya Kwanza Feb 5-6, Marudiano Feb 12-13
Real Sociedad/Real Racing Santander v Levante/FC Barcelona
RCD Espanyol/Real Madrid v Atlético de Madrid/Athletic de Bilbao
FAINALI
Aprili 19
0 comments:
Post a Comment