Tuesday, 31 December 2013

MBUNGE MSINGWA ASEMA ZITTO KABWE SI MAARUFU KULIKO CHADEMA

  AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA RASMI YA KATIBA MPYA

Wananchi wa jimbo la Iringa mjini  wakiwa katika mkutano wa mbunge Peter Msigwa leo 

Mbunge wa  jimbo al Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwahotubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini  leo katika uwanja  wa Mwembetogwa .


...................................................................................................
MBUNGE  wa  jimbo la  Iringa  mjini mchungaji peter Msigwa amemshukia  mbunge wa  jimbo  la Kigoma  kaskazin Bw  Zitto kabwe  kuwa  si  maarufu kuliko Chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema)  huku  akiwapongeza  mawaziri  watatu  wa  JK akiwemo naibu waziri wa maji Dr  Binilith Mahenge na waziri  wake  Jumanne Maghembe  kuwa  si mawaziri mizigo ndani ya baraza la   mawaziri wa serikali ya  Kikwete.

 Mbali ya  kuwapongeza  mawaziri hao  pia   mbunge Msingwa amempongeza waziri wa ujenzi Dr John Magufuli  kuwa amekuwa akifanya kazi vema na  kumpongeza Rais Dr Jakaya  Kikwete  kwa kukamilisha mchakato    na msimamo wake juu ya rasmi mpya  ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa  Tanzania.

Mbunge  Msingwa akiwahutubia  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini leo katika  viwanja vya Mwembetogwa  alisema  kuwa mbali ya CCM kuwaona  baadhi ya mawaziri  wa chama chao ni mizigo ila kwa upande wake anapenda kuwapongeza  baadhi  ya  mawaziri ambao  utendaji kazi wao unaonekana  akiwemo    waziri wa wizara ya maji na  naibu wake ,waziri wa ujenzi na  waziri wa mazingira  ambao wameonyesha  msimamo wa kweli katika  kuwatumikia  wananchi .

katika hatua nyingine  mbunge Msigwa  amemshukia  aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema Bw   kabwe kuwa anatafuta umaarufu binafsi  kuliko  kujijenga chama  chake na  kuwa  Kabwe hana nia njema  na Chadema na  kuwataka  wanachadema jimbo la Iringa mjini  kutomsikiliza Zitto kabwe kwa lolote .

Kwani  alisema  kuwa mwanachama na kiongozi mzuri ni  yule ambae  anafanya kazi ya  kukijenga  chama na  si kujijenga  yeye binafsi na kuwa anachofanya  Zitto ni  udhaifu mkubwa  na  hapaswi kuachwa kuendelea  kulisha  watu maneno ya  kuua  chama.

Alisema  kuwa iwapo  Zitto  leo  hataki kumusikiliza mwasisi wa Chama  hicho mzee Mtei  wala  kuwasikilizA  viongozi wa juu wa chama  hicho akiwemo  mwenyekiti wa katibu mkuu ni  wazi hakitakii mema  Chadema na wana  Chadema hawana budi kumpuuza kiongozi na mwanachama yeyote mwenye lengo la kuua chama.

Mbunge Msigwa aliwataka   wananchi wa jimbo la Iringa mjini  kunyosha  mikono juu kwa wale ambao  wanataka Zitto kabwe kufukuzwa ndani ya  chama na umati wote uliokuwepo uwanjani hapo ulinyosha mikono  kukubali aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Bw kabwe  kuondolewa .

Kuhusu rasmi  ya katiba   Mbunge  Msigwa alimpongeza  rais Kikwete  kuwa ameonyesha ushujaa wa hali ya juu  katika kupigania  upatikanaji wa katiba mpya  na  kuwa  iwapo  wabunge wa CCM watapinga  wao kama  Chadema  watarudi kwa wananchi   kuhamasisha ile  kupiga kura ya kuikataa  katiba  itakayopendekezwa na wabunge wa CCM.

Pia  mbunge Msigwa amewachana viongozi wa CCM akiwemo katibu mkuu wake na katibu wa itikadi na uenezi  kuwa ni wanafiki  wakubwa ambao  leo  wameteka   hoja ya  Chadema na  kuwapinga   mawaziri mizigo.

0 comments: