Sunday, 29 December 2013

KATIBA MPYA : MWELEKEO MPYA KUJULIKANA LEO SAA 6 MCHANA

 



Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakitia saini Rasimu ya Pili ya Katiba juzi. Rasimu hiyo itakabidhiwa leo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein, Karimjee, Dar es Salaam. Picha ya mtandao. 

Dar es Salaam. Swali la nini kilichomo katika Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya litajibiwa leo wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakapokabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.
Rasimu inayosubiriwa kwa hamu na wananchi wa kada zote itatolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo ilijadiliwa na kuboreshwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyoketi kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, mwaka huu.
Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotangazwa Juni 4, mwaka huu.
Hafla ya kukabidhi rasimu hiyo itafanyika leo saa 6.00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na asasi mbalimbali
.Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

0 comments: