Monday, 30 December 2013

RAIS JK AKABIDHIWA NAKALA YA RASMU YA KAIBA MPYA

Nakala ya Rasimu ya Katiba aliyokabidhiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein leo, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, imepachikwa baada ya picha zifuatazo zinazoambatana na tukio husika.

Hatua inayofuata baada ya kukabishiwa kwa rasimu hiyo ni kuundwa kwa Bunge Malumu la Katiba ambalo wito umeshatolewa kwa makundi mbalimbali kuteua wawakilishi, kisha itajadiliwa na Bunge hilo kabla ya hatua ya kupiga kura ya maoni kufuata katika kutafuta Katiba Mpya ya Tanzania iliyopangwa kupatikana kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2015.

warioba 

Kwa kifupi kuhusu Rasimi ya pili ya mabadiliko ya katiba
Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza in ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240 .Wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora  kama  ifuatavyo:
1-lugha ya kiswahili ni Lugha ya Taifa.
2-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
3-Wabunge wasiwe mawaziri
4-Kuwe na ukomo wa wabunge
5-Wananchi wawajibishe wabunge
  6-Spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.
7-Kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa. 
MUUNGANO
Muungano umependekezwa uwe wa serikali tatu kutokana  na  kero  mbalimbali  zilizoko pande zote mbili.
Baadhi ya kero hizo ni kama ifuatavyo:  
Kero za wazanzibar
  1-Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania na hivyo kutumia mwanya huo kujipatia misaada toka nje
2-Mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
 3-Kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais   
Kero za  Tanzania Bara.
   1-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
 2-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar  wakati wazanzibar huku Tanganyika wanaruhusiwa




RAIS KIKWETE, DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA LEO


 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.
Jaji Warioba akikabidhi rasimu hiyo pia kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti  wa NCCR Mageuzi,  James Mbatia.
Rais Jakaya Kikwete, Dk. Shein, Dk. Bilal, Maalim Seif Sharif Mahad na viongozi wengine wakiwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba


0 comments: