Friday, 27 December 2013

OPERATION TOKOMEZA UJANGIRI: WAONAVYO FILIKUNJOMBE, ITUTU, SHIBUDA NA WENGI

 Mheshimiwa mbunge wa Ludewa filikunjombe (katikati) picha na Maktaba
Makala hii imenukliwa kutoka kwenye gazeti la JAMHURI “Kitanzi cha JK
Rais Jakaya Kikwete, akiwa anatarajiwa kulisuka upya Baraza la Mawaziri, kuna kila dalili kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sasa ndio imebaki kuwa kitanzi kinachotishia uhai wa Serikali yake.

Wakati mwaka 2011 Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa inaongoza kwa kupigiwa kelele, baada ya wizara hiyo kushikwa na Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi, sasa imetulia ila Maliasili ni tatizo.

Ukubwa wa tatizo la Wizara ya Maliasili unadhihirishwa na idadi kubwa ya mawaziri walioachia ngazi katika wizara hiyo, watendaji walioondolewa na jinsi wafanyabiashara wanavyoikodolea macho.

Kwa upande mwingine, wakati ikionekana wizara hiyo kuwa ni ngumu, Naibu Waziri mmoja amewaita wadau wake,


 

0 comments: