Friday, 6 December 2013

KESI YA MAKUNGA NA WENZAKE LEO

 
Dar es Salaam.Kesi ya makala ya uchochezi inayomkabili Meneja Uendelezaji na Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), inayochapisha Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, Theophil Makunga na wenzake wawili, leo itatajwa na kupangiwa tarehe ya hukumu.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema anatarajiwa kuitaja kesi hiyo na kuipangia tarehe ya hukumu.
Makunga ambaye ni mshtakiwa wa tatu na wenzake Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, mwishoni mwa wiki iliyopita waliwasilisha majumuisho yao ya mwisho mahakamani hapo wakiiomba mahakama iwaone hawana hatia, katika kesi hiyo.
Makunga aliunganishwa katika kesi hiyo kutokana na kampuni yake kuchapisha gazeti la Tanzania Daima likiwa na makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi, wakati alipokuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MCL.
Gazeti hilo la Novemba 30, 2011, lilikuwa na makala iliyokuwa na Kichwa cha Habari, “Waraka Maalumu kwa Askari Wote,” iliyoandikwa na mwandishi wa safu ya Kalamu ya Mwigamba, Samson Mwigamba.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uchochezi.

CHANZO Na Tausi Ally, Mwananchi

0 comments: