Sunday, 8 December 2013

TAARIFA YA IGP YAUTEUZI WA MAKAMANDA WA POLISI WA MBEYA ,SIMIYU NA MWANZA

IGP SAIDI MWEMA PICHA NA MAKITABA YETU
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amefanya uteuzi wa Makamanda wa Polisi kwa Mikoa mitatu Mwanza, Mbeya na Simiyu, ambapo amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi mkoa 
wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)  Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

Aidha, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim amehamishiwa Kanda Maalum ya  Dar es Salaam  kuwa Mkuu wa Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam  amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion  Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi  wa mkoa wa Tarime Rorya amehamishiwa  Tunduru kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

 

0 comments: