Sunday, 29 December 2013

HILI NDIO BAO LA USHINDI LA CHELSEA KUPITIA SAMUEL ETO'OO STAMFOED BRIDGE

Shujaa; Samuel Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi, Chelsea ikiilaza Liverpool 2
KOCHA Mreno Jose Mourinho ametoka na furaha Uwanja wa Stamford Bridge jioni hii, baada ya timu yake, Chelsea kuilaza mabao 2-1 Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Shukrani kwake mshambuliaji mkongwe, Samuel Eto'o aliyefunga bao la ushindi dakika ya 34 akimalizia pasi ya Oscar ndani ya sita.
Mabeki wa Chelsea walimchezea 'kindava' mshambuliaji Luis Suarez na akatoka uwanjani bila kufunga bao.

Liverpool ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne, mfungaji Skrtel, lakini Edin Hazard akasawazisha dakika ya 17.
Kwa ushindi huo, Chelsea inatimiza pointi 37 na kubaki nafasi ya tatu, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 36.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Tottenham Hotspur imeifunga Stoke City mabao 3-0, wafungaji Soldado dakika ya 37, Dembele dakika ya 65 na Lennon dakika ya 69.

Ushindi raha; Lennon kulia akishangilia Adebayor baada ya kuifungia Spurs katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke Jana

0 comments: