>>SIMBA v AFC LEOPARDS, KMKM v KCC!
RATIBA:
Jumatano Januari 1
KMKM v KCC [Saa 10 Jioni, Amaan Stadium, Zanzibar]
Simba v AFC Leopards [Saa 2 Usiku, Amaan Stadium, Zanzibar]
MAPINDUZI
CUP, Kombe la Kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, litaanza
kushindaniwa Jumatano Januari Mosi huko Amaan Stadium, Zanzibar na
Gombani Stadium, Pemba na Timu 12 zinatarajiwa kushiriki.
Wenyeji Zanzibar wanawakilishwa na Timu 4 ambazo ni KMKM, Chuoni, Spice Stars na Clove Stars.
Tanzania Bara ina Timu 4 ambazo ni Mabingwa Yanga, Simba, Azam na Mbeya City.
Timu kutoka nje ya Tanzania ni 4 nazo ni URA na KCC za Uganda na AFC Leopards na Tusker za Kenya.
Timu hizo zimegawanywa katika Makundi
Matatu ya Timu 4 kila moja na Timu mbili za Juu toka kila Kundi pamoja
na Timu mbili zitakazomaliza Nafasi ya Tatu Bora zitasonga
MFUMO:
Makundi:
-KUNDI A: Mbeya City, Clove Stars (Kombaini ya Pemba), Chuoni, URA (Uganda)
-KUNDI B: Simba, KMKM, AFC Leopards (Kenya), KCC (Uganda)
-KUNDI C: Azam, Tusker (Kenya), Yanga, Spice Stars (Kombaini ya Zanzibar)
**Robo Fainali Jumatano Januari 8.
**Nusu Fainali Ijumaa Januari 10
**Fainali Januari 13.
Katika Mechi za fungua dimba hapo kesho,
zitakazochezwa Mjini Zanzibar Uwanja wa Amani, Wenyeji KMKM wataanza na
KCC ya Uganda na kufuatiwa Usiku na Mechi kati ya Simba na AFC Leopards
ya Kenya.
Mashindano haya yataendelea Alahamisi kwa Mechi nne.
RATIBA:
Alhamisi Januari 2
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Spice Stars v Azam [Saa 10 Jioni]
Yanga v Tusker [Saa 2 Usiku]
[Gombani Stadium, Pemba]
URA v Chuoni [Saa 8 Mchana]
Mbeya City v Clove Stars [Saa 10 Jioni]
**RATIBA KAMILI TUTALETA BAADAE
0 comments:
Post a Comment