Baada
ya taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
kutangazwa usiku wa manane kuamkia leo, niliamini kuwa magazeti ya
Tanzania yatakuwa yalishafunga mitambo na hivyo shughuli zao za
kuchapisha taarifa hii zitafanyika leo na hivyo kuonekana mitaani kesho.
Binafsi niliwaambia rafiki zangu kuwa ninatamani sana kusoma vichwa vya magazeti ya Tanzania kwa siku ya leo ili kufahamu ni magazeti gani yameweza kuvunja ratiba yao na kuwa radhi kuchapisha habari hii kubwa, wachilia mbali hata kama gazeti litachelewa kutoka. Niliambiwa kwa kweli magazeti yaliyoonekana kuvuruga ratiba na kila kitu ili kuhakikisha yanachapisha habari hiyo ili iwafikie wananchi leo, ni RAI na MWANANCHI.
Nimesoma vivyo pia kwenye blogu ya Muhidini Issa Michuzi, hivyo sina budi kuungana na Watanzania wote wanaopongeza magazeti haya kwa kwenda 'above and beyond your line of duty!'

0 comments:
Post a Comment