Baadhi
ya wakazi wa mjini Singida, wakiwa wamekusanyika katika duka la wakala
wa M-pesa lililopo kwenye taasisi ya elimu ya watu wazima, muda mfupi
baada ya mmiliki wa duka hilo Mashaka Omari Makiya,kujipiga risasi kwa
kutumia Bastola yake na kusababisha kifo chake.
Mwandishi
wa habari wa radio na TV Clouds mkoani Singida, John,akisoma wosia
(haupo kwenye picha) ulioachwa na mfanyabiashara Mashaka Omari
Makiya,aliyejiua kwa kujipiga risasi kwa bastola yake.Wosia huo umedai
kuwa wadogo wa marehemu wakabidhiwe nyumba na fedha alizoziacha.(Picha
na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Mashaka
maarufu kwa jina la Mashakom, amejipiga risasi kwa kutumia bastola yake
aina ya ‘silencer’ usiku wa Desemba 27 mwaka huu, nyumbani kwake Ipembe
mjini hapa.
Shuhuda
wa tukio hilo,Shija John amesema Desemba 28 mwaka huu saa saba mchana
askari polisi walifika nyumbani kwa marehemu iliyopo mkabala na nyumba
ya kulala wageni ya Meatu eneo la Ipembe.
Amesema
askari polisi hao waliingia chumbani kwa Mashaka ambapo walikuta mwili
wa mfanyabiashara huyo ukiwa sakafuni.Pia walikuta bastola yake ikiwa
pembeni mwa mwili huo pamoja na simu zake tatu.
“Taarifa
nilizonazo ni kwamba mfanyakazi wa Mashaka aligundua tukio hilo na
kisha alitoa taarifa kituo kikuu cha kati cha polisi na askari walifika
mara moja”,amesema.
Katika
hatua nyingine, mwandishi wa habari hizi aliweza kufika kwenye moja ya
maduka yake matatu ya M-pesa na kushuhudia ujumbe wa maandishi ulioachwa
na Mashaka ndani ya gari lake jeusi.
Pamoja
na askari polisi kukataa kutoa kibali kwa waandishi habari kusoma
ujumbe huo au kuupiga picha,watu waliobahatika kuusoma ukiwa ndani ya
gari wamedai kuwa marehemu amemhusisha na kifo chake mfanyabiashara
mmoja (jina tunalo) aliyekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara pia
marehemu Mashaka ameagiza kuwa nyumba na fedha zake wapewe wadogo zake.
Kifo
cha Mashaka kimezua hofu kubwa na kazi ya uwakala wa M-pesa kwa madai
kwamba katika miaka michache waliokuwa wafanyabiasha wa uwakala
huo,Tembs na Rweyemamu wote wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema bado hajapata
taarifa hizo na ameahidi kulifuatilia na kutoa habari ili jamii iweze
kujua kilichojiri.
0 comments:
Post a Comment