Saturday, 7 December 2013

MAJANGA KWA MAN UNITED, YAFUNGWA TENA NYUMBANI OLD TRAFFORD!!

>>NI MARA YA KWANZA KUFUNGWA OLD TRAFFORD 2 MFULULIZO KWENYE LIGI TANGU 2002

>>NI MARA YA KWANZA NEWCASTLE KUSHINDA OLD TRAFFORD TANGU 1972

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 7
Man United 0 Newcastle 1
1800 Crystal Palace v Cardiff
1800 Liverpool v West Ham
1800 Southampton v Man City
1800 Stoke v Chelsea
1800 West Brom v Norwich
BPL2013LOGO
2030 Sunderland v Tottenham

Manchester United leo wamepata kipigo chao cha pili mfululizo cha Ligi Uwanjani kwao Old Trafford na hii ni mara ya kwanza tangu Mwaka 2002 wakati Newcastle waliposhinda Bao 1-0 na hii ni mara ni mara ya kwanza kwa Newcastle kushinda Uwanjani hapo tangu Mwaka 1972.
Bao la ushindi la Newcastle lilifungwa na Yohan Cabaye katika Dakika ya 61.
Man United, ambao leo walibadilisha Wachezaji 7 toka Kikosi kilichofungwa Jumatano, walipata nafasi kadhaa za kufunga pale Patrice Evra alipopiga kichwa na Mpira kupiga posti na nyingine ni majaribio ya Javier Hernandez na Adnan Januzaj yaliyookolewa na baadae Bao la Robin van Persie kukataliwa kwa kuwa Ofsaidi.
Jumatano iliyopita Man United walifungwa Old Trafford na Everton Bao 1-0 na Mechi inayofuata kwao ni hapo Jumanne Desemba 10 watakapocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Uwanjani Old Trafford na Shakhtar Donetsk.

MAN UNITED==ZINAZOFUATA:
10 Des Man Utd v Shakhtar UCL
15 Des Aston Villa v Man Utd LKE
18 Des Stoke v Man Utd LC
21 Des Man Utd v West Ham LKE
26 Des Hull v Man Utd LKE
28 Des Norwich v Man Utd LKE
1 JAN Man Utd v Tottenham LKE

Jumapili Desemba 15, Man United wapo Ugenini Villa Park kucheza na Aston Villa.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Nani, Cleverley, Jones, Januzaj, van Persie, Hernandez
Akiba: Ferdinand, Anderson, Lindegaard, Young, Welbeck, Valencia, Zaha.
Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Coloccini, Santon, Cabaye, Tiote, Anita, Sissoko, Remy, Gouffran
Akiba: Cisse, Ben Arfa, Yanga-Mbiwa, Gutierrez, Elliot, Shola Ameobi, Obertan.
Refa: Andre Marriner

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili Desemba 8
1630 Fulham v Aston Villa
1900 Arsenal v Everton
Jumatatu Desemba 9
2300 Swansea v Hull

MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 14 19 34
2 Chelsea 14 14 30
3 Man City 14 26 28
4 Liverpool 14 13 27
5 Everton 14 9 27
6 Newcastle 15 -1 26
7 Tottenham 14 -2 24
8 Southampton 14 5 22
9 Man Utd 15 3 22
10 Aston Villa 14 0 19
11 Swansea 14 1 18
12 Hull 14 -6 17
13 West Brom 14 -2 15
14 Stoke 14 -6 14
15 Cardiff 14 -9 14
16 Norwich 14 -16 14
17 West Ham 14 -3 13
18 Fulham 14 -14 10
19 Crystal Palace 14 -14 10
20 Sunderland 14 -17 8

0 comments: