Uongozi
wa klabu ya Young Africans umewasilisha barua rasmi kwa ZFA kutoshiriki
mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
kesho Januari Mosi 2014 Visiwani Zanzibar katika miji ya Unguja na
Pemba kutokana na kuamua kulivunja benchi nzima la Ufundi.
Kufuatia
kupewa taarifa (notice) kwa kocha msaidzi Fred Felix “Minziro” kocha wa
makipa Razaki Siwa na daktari wa timu Nassoro Matuzya kwa sasa Young
Africans haina kiongozi wa benchi la ufundi hali inayopelekea timu
kujitoa katika mashindano hayo.
Wiki
iliyopita mholanzia Ernie Brandts alipewa taarifa (notice) ya siku
thelathini (30) na klabu ya Young Africans kusitisha mkataba wake na
timu ilikuwa chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa
makipa Razaki Siwa ambao nao pia wamepewa taarifa za kusitisha ajira
zao.
Kutokana
na timu kwa kwa sasa kutokua na kocha mkuu, kocha msaidizi, kocha wa
makipa na dakatari wa timu imekua ni vigumu kwa kikosi cha Young
Africans kwenda kushiriki mashindano hayo kwani haina mwalimu hata mmoja
kwa sasa.
Hii
inafuatia uongozi wa klabu ya Young Africans kuamua kufanya mabadiliko
ya benchi zima la Ufundi kwa lengo la kuongeza tijaa katika utendaji na
kuhakikisha benchi linapata watu wa kuchukua nafasi zao na kuanza kazi
mara moja.
Aidha
uongozi unaendelea na mchakato wa kuwapata warithi watakaochukua nafasi
hizo haraka ili waweze kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom na mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Idadi
ya makocha waliotuma maombi ya kuomba kuinoa timu ya Yanga mpaka sasa
ni 45 huku pia idadi hiyo ikiendelea kuongeza kadri siku zinavyokwenda
na uongozi unaamini utapata makocha wazuri, wenye uwezo mkubwa pia wa
kuifikisha Yanga katika hatua nyinge ya juu zaidi.
0 comments:
Post a Comment