LIVERPOOL YASHINDA MECHI YA BAO 3 ZA KUJIFUNGA WENYEWE!!
STOKE YAISAMBARATISHA CHELSEA KWA MARA YA KWANZA BAADA MIAKA 38!!
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Desemba 7
Man United 0 Newcastle 1
Crystal Palace 2 Cardiff 0
Liverpool 4 West Ham 1
Southampton 1 Man City 1
Stoke 3 Chelsea 2
West Brom 0 Norwich 2
[Saa za Bongo]
2030 Sunderland v Tottenham
+++++++++++++++++++++++++
WEST BROM 0 NORWICH 2
Bao mbili za Gary Hooper na Leroy Fer
zimewapa Norwich ushindi wa Ugenini wa Bao 2-0 na kuchupa juu ya West
Bromwich katika Msimamo wa Ligi.
VIKOSI:
WBA: Myhill, Jones, McAuley, Lugano, Ridgewell, Yacob, Mulumbu, Amalfitano, Sessegnon, Brunt, Anichebe.
Norwich: Ruddy; Whittaker, Turner, Bassong, Olsson; Redmond, Howson, Johnson, Fer, Elmander, Hooper.
STOKE 3 CHELSEA 2
Kipigo hiki ni cha kwanza kwa Chelsea
toka kwa Stoke City kwa Miaka 38 na Bao lililoiua Chelsea lilifungwa na
Mchezaji alietoka Benchi Oussama Assaidi ambae alifunga katika Dakika ya
90.
Bao za Stoke zilifungwa na Peter Crouch,
Dakika ya 42, Stephen Ireland, 50 na Assaidi, 90 na Chelsea kupata Bao
zao mbili zote kupitia Schürrle Dakika ya 9 na 53.
VIKOSI:
Stoke: Begovic; Cameron, Shawcross, Huth, Muniesa; Walters, Nzonzi, Whelan, Adam, Arnautovic; Crouch.
Chelsea: Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Ramires, Mikel; Hazard, Mata, Schurrle; Torres.
CRYSTAL PALACE 2 CARDIFF 0
Cameron Jerome aliifungia Crystal Palace
Bao lake la kwanza kwa Klabu hiyo na Marouane Chamakh kupiga Bao la
Pili na kuipa Palace ushindi wa Bao 2-0 ukiwa ni ushindi wao wa pili
mfululizo na hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo kwenye Ligi Kuu tangu
Mwaka 2004.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Dikgacoi, Jedinak, Bannan, Puncheon, Chamakh, Jerome.
Cardiff: Marshall, Theophile-Catherine, Caulker, Turner, John, Medel, Bo-Kyung, Whittingham, Mutch, Cowie, Campbell
LIVERPOOL 4 WEST HAM 1
Hii ni Mechi ambayo Bao 3 zilikuwa za kujifunga wenyewe wakati Liverpool wanaichapa West Ham Bao 4-1 Uwanjani Anfield.
Liverpool walitangulia kupata Bao katika
Dakika ya 42 kwa Guy Demel kujifunga mwenyewe na Mamadou Sakho kuipa
Bao la pili kisha Martin Skrtel akajifunga mwenyewe na kuipa West Ham
Bao 1.
Likafuata Bao la Luis Suarez na jingine
la Joey O'Brien kujifunga mwenyewe na kuipa Liverpool ushindi wa Bao 4-1
ambao umewafanya wakamate Nafasi ya Tatu kwenye Ligi.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet, Flanagan, Sakho, Skrtel, Johnson, Allen, Gerrard, Henderson, Sterling, Coutinho, Suarez.
West Ham: Jaaskelainen, Demel, McCartney, Collins, Tomkins, Noble, Diame, Nolan, Downing, Jarvis, Maiga.
SOUTHAMPTON 1 MAN CITY 1
Bao murua la Dani Osvaldo katika Dakika
ya 42 limewapa Southampton Sare ya Bao 1-1 na Manchester City ambao
wameonyesha tena hawana ubavu kwenye Mechi za Ugenini.
Sergio Aguero ndie aliefunga Bao kwa Man City katika Dakika ya 10 kutokana na krosi ya Aleksandar Kolarov
VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Chambers, Fonte, Lovren, Shaw, Cork, S. Davis, Ward-Prowse, Lallana (c), Rodriguez, Osvaldo.
Manchester City: Pantilimon, Zabaleta, Kompany (C), Demichelis, Kolarov, Milner, Yaya Toure, Fernandinho, Nasri, Aguero, Negredo.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili Desemba 8
1630 Fulham v Aston Villa
1900 Arsenal v Everton
Jumatatu Desemba 9
2300 Swansea v Hull
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 14 | 19 | 34 |
2 | Liverpool | 15 | 16 | 30 |
3 | Chelsea | 15 | 13 | 30 |
4 | Man City | 15 | 26 | 29 |
5 | Everton | 14 | 9 | 27 |
6 | Newcastle | 15 | -1 | 26 |
7 | Tottenham | 14 | -2 | 24 |
8 | Southampton | 15 | 5 | 23 |
9 | Man Utd | 15 | 3 | 22 |
10 | Aston Villa | 14 | 0 | 19 |
11 | Swansea | 14 | 1 | 18 |
12 | Stoke | 15 | -5 | 17 |
13 | Hull | 14 | -6 | 17 |
14 | Norwich | 15 | -14 | 17 |
15 | West Brom | 15 | -4 | 15 |
16 | Cardiff | 15 | -11 | 14 |
17 | West Ham | 15 | -6 | 13 |
18 | Crystal Palace | 15 | -12 | 13 |
19 | Fulham | 14 | -14 | 10 |
20 | Sunderland | 14 | -17 | 8 |
0 comments:
Post a Comment