Saturday, 28 December 2013

LORI LA MAFUTA LAKAMATWA LIKISAFIRISHA VIPODOZI HATARI


Click image for larger version. 

Name:	ImageUploadedByJamiiForums1388224633.977310.jpg 
Views:	0 
Size:	205.0 KB 
ID:	129076

JESHI la  polisi  mkoa  wa  Iringa  limewakamata  watu  wawili  akiwemo  dereva  wa tenki  la  mafuta  lenye namba za usajili  T 247 BHP  wakisafirisha shehena  ya   vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani ya tenki  hilo la mafuta  kutoka nchi  za  kusini  mwa Tanzania  kuelekea  jijini  Dar es Salaam .(P.T)
Kamanda  wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi  alisema  kuwa  lori hilo lenye namba za usajili  T 247 BHP  likiwa na tela  lenye namba T 598 BMK   ni mali ya kampuni ya  World OIL Ltd  ya  Jijini Dar es Salaam lilikuwa  likiendeshwa na  Mohamed  Sadru (23) mkazi  wa  Mbezi Temboni jijini  Dar es Salaam .

 Mbali  ya  dereva   huyo  pia  jeshi  hilo  linamshikilia mfanyabiashara  aliyekuwa akisafilisha  mzigo  huo  Bw Kassim Kaifa (23) mkazi  wa jijini Dar es Salaam  kwa tuhuma  za  kuhusika na mzigo  huo.

Kamanda Mungi  aliwaeleza  wanahabari  leo    kuwa  mtego wa jeshi  la  polisi  uliweka  baada ya  kupokea  taarifa  kutoka kwa rai  wema kuhusiana na lori  hilo kutumika isivyo  kwa kusafirisha vipodozi  hivyo.

Alisema  kuwa  taarifa  kuhusiana na lori  hilo kusafirisha vipodozi  badala ya  mafuta   waliitapata  kutoka  jana  na mtego  wa  kulikamata  lori hilo  umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri  ya leo 

Hata   hivyo  alisema  kuwa  sehemu  kubwa ya  vipodozi  hizo   ni  vile  ambavyo vilipigwa marufuku na  serikali kutokana na kuwa na madhara  makubwa kwa afya  ya  watumiaji  wa vipodozi  hivyo.

Alisema  kuwa  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kumata  vipodozi hivyo kwa  kushirikiana na mamlaka ya  chakula na  dawa ,wakala  wa  barabara  mkoa  wa Iringa  na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) 

Kamanda huyo  alisema kuwa  watuhumiwa hao   watafikishwa mahakamani  mara  baada ya  uchunguzi  kukamilika na  kuwa ni mapema  kwa  sasa  kuitaja thamani  ya vipodozi  hivyo na  nchi  ambayo lori  hilo  lilikuwa  likitoka kutokana na sababu  za kiusalama.
MWISHO
 Na Francis Godwin Blog

0 comments: