Thursday, 26 December 2013

HUYU NDIE MWANAFUNZI WA CHUO CHA CBE-DODOMA AFARIKI DUNIA.

DSC05139 b94c3
MAREHEMU SAMWEL P. KITULA

Ikiwa
ni siku moja imepita Tangu Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma
kiondokewe na aliye wahi kuwa Mwanafunzi wa Chuo hicho katika Level ya
Diploma 2012/2013 Marehemu Zeinabu J. Kasenga (ODMK -2012/2013)
Simanzi zimezidi kutanda Chuoni hapa baada ya Mwanafunzi Mwingine Bw. Samwel P. Kitula (37)
aliyekuwa akisoma Bachelor Degree in Procurement and Supplies
Management mwaka wa tatu (3) mkondo "A" Kufariki Dunia usiku wa
kuamkia Tarehe 26/12/2013 ( Mnamo saa 8 usiku) katika hospitali ya
Mkoa wa Dodoma (General Hospital).
Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia amesema Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Matatizo ya Ini mpaka kupelekea Mauti yake.
Kwa
upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma Mhe. Remidius M. Emmanuel amesema
Amepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa sana na kuwataka wanafunzi
wote kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza
mwanafunzi mwenzetu. Hata hivyo Rais huyo amewataka wanafunzi kuwa
watulivu wakati taratibu mbalimbali zinaendelea na kila
kitakachoendelea watafahamishwa kupitia taratibu mbalimbali za
mawasiliano hapa chuoni.Ingawa amasema Marehemu amekuwa akiishi na
familia yake eneo la Makole karibu kabisa na Lodge ya ELGON, hivyo ni
vema kila mtu kwa nafasi yake kujongea eneo hilo kwa ajili ya kutoa
pole kwa Familia ya Marehemu.

0 comments: