Monday, 30 December 2013

WAUGUZI WASABABISHA MAMA KUJIFUNGUA NJE YA HOSPITAL MKOAN MBEYA

Picture
Sabina Mwakyusa (28) anayedai alifukuzwa na wauguzi wodini na kujifungulia nje ya geti usiku huku mvua ikinyesha akiwa na Mama yake mzazi, Rhoda Mwakyusa(50) aliyembeba mwanaye huyo aliyezaliwa. (picha: Kalulunga blog)
Na Gordon Kalulunga, Mbeya -- HOSPITALI teule ya wilaya ya Mbeya (Ifisi-Mbalizi), imekumbwa na kashfa ya kufukuza wajawazito wodini kisha wajawazito hao kujifungulia katika mazingira yasiyo na staha nje ya hospitali.

Tukio la hivi karibuni limetokea usiku wa Desemba 19, mwaka huu, ambapo baadhi ya wauguzi waliokuwepo katika chumba cha matazamio ya kujifungua, wanadaiwa kumfukuza na kumpiga mjamzito Sabina Mwakyusa (28) mkazi wa Kijiji cha Iwala, kata ya Utengule Usongwe wilayani humo.

Akizungumza na Kalulunga media blog, Sabina, alisema alifika hospitalini hapo Desemba 18, mwaka huu na alipimwa na 


0 comments: