MATUKIO YA MTWARA, HALI YA USALAMA BADO TETE.
ASKARI WATUHUMIWA KUBAKA NA KUUWA MAMA MJAMZITO INASEMEKANA WANAFANYA MAKUSUDI ILI KULIPIZA KISASI
Hali ya usalama katika Manispaa ya
Mtwara Mikindani mkoani hapa imezidi kuwa mbaya baada ya askari polisi
kudaiwa kufanya unyama kwa kuwabaka wanawake na kumpiga risasi mjamzito
Mbali na unyama huo polisi pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba tatu za wananchi katika mtaa wa Magomeni na vibanda vya maduka kadhaa na kupora vitu vilivyomo ndani.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa anasema hali ni shwari na kwamba wananchi watoke nje kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi amethibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, zinazoaminika kuwa za risasi na hivyo kufanya idadi ya maiti zilizopokelewa hospitalini hapo kufikia mbili na majeruhi 18:
“Ni kweli kwa leo( jana) tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba, amepigwa risasi tumboni.pia tumepokea mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chuno, amevunjwa miguu yote kwa risasi.”

Habari zinadai kuwa mjamzito huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake baada ya polisi kuvamia makazi yake.
Huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyo wazi, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya, sauti za milio ya mabomu na bunduki zimetawala, wanajeshi waliovalia sare wameuzingira mji wakiwa katika magari na pikipiki.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti wakazi hao wamelalamikia kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuingia katika makazi yao, kuwapiga, kuwabaka na kuwapora mali zao:
“Magomeni A
hatuna amani askari wanaingia majumbani mwetu wanatupiga na
kutunyang’anya simu, yani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepoteza
watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi” alisema Paulina Idd na kuongeza:
“Majumba yetu yamechomwa moto , wanaofanya fujo ni polisi wenyewe halafu wanakuja wanatubaka na kuiba mali zetu halafu tunateseka sisi yaani tumechoka kabisa na serikali yenyewe,” alisema Paulina.
“Majumba yetu yamechomwa moto , wanaofanya fujo ni polisi wenyewe halafu wanakuja wanatubaka na kuiba mali zetu halafu tunateseka sisi yaani tumechoka kabisa na serikali yenyewe,” alisema Paulina.
Kamanda Sinzumwa alipoulizwa kuhusiana
na tuhuma hizo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa
atapingana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Mchimbi aliyewasili
Mtwara leo: “Kuhusiana na suala hilo siwezi
kulizungumzia kwa sasa kwani nitapingana na Waziri wangu kwani leo
ametoa tamko bungeni na leo atawasili,” alieleza Sinzumwa
Wananchi wazungumzia bajeti
Wakizungumzia uwasilishwaji wa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini wakazi wa hapa wamesema kuwa hawakubaliani na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwani mpango huo utawaletea dhuluma:
“Mpango wa kusafirishwa kwa gesi asilia hatuna mpango nao kwa wakazi wote wa Mtwara kwa kifupi akina mama wa mtwara hatutaki itoke,” alisema Fatuma Abdallah.

******************************************************
Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya
wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali
ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za
kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo
asubuhi katika eneo hilo..
0 comments:
Post a Comment