Wednesday, 15 May 2013

AKAMATWA KWA TUHUMA UTAWA BANDIA

Picture
 Mtuhumiwa Phylis Wanjiru
 
via DEMASHO blog:

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa ma-sister wa Kanisa Katoliki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya ma-sister wengine kubaini kuwa si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila lake ni Muwembu wa Kituo nchini Kenya amekamatwa majira ya saa kumi jioni tarehe 13, Mei, 2013 katika nyumba hizo za ma-sister zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha, Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali alikataa kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya laini (line/chip) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (passport) mbili, moja ikiwa 


S

0 comments: