Wednesday, 22 May 2013

Kauli na picha za Profesa Jay baada ya kujiunga Chadema


Jay akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Mbeya, Mh. Joseph "Sugu" Mbilinyi
Jay akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Mbeya, Mh. Joseph “Sugu” Mbilinyi


Sugu, Prof Jay, na John Mnyika
Sugu, Prof Jay, na John Mnyika


profesa-jay-chadema-picha-2
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ukipenda wa Mitulinga, ametangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo alikabidhiwa kadi yake leo Mjini hapa. Kadi hiyo alikabidhiwa na Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA), Joseph “Sugu” Mbilinyi mbele ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika na wakereketwa wengine wa chama hicho.
Prof. Jay amesema amepata baraka za wazazi wake wote wawili za kujiunga CHADEMA bila ya kushawishiwa na yeyote, bali kwa kufuata maamuzi yake mwenyewe baada ya kuelewa sera na harakati za CHADEMA ambazo ndizo zilizomvutia na kumashawishi kujiunga. Pia, harakati zake binafsi zimelandana na za chama hicho, kwa kuwa anaendelea kulikomboa taifa kwa njia ya muziki.

0 comments: