Sitta awataja marafiki wanaotetea nchi kwa haki
Na Sheilla Sezzy, Mwananchi
Mwanza. Katika kile kinachoonekana ni mbio za
urais 2015, makada wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameunganisha
nguvu tayari kwa kinyang’anyiro hicho.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta ni kama ametangaza timu yake ingawa si rasmi pale alipoweka
hadharani majina ya makada hao akisema kuwa ni marafiki zake wa karibu
ambao wana mikono misafi.
Sitta ambaye anatajwa kuwa mmoja wa makada
watakaowania urais 2015, aliwataja marafiki zake hao juzi wakati wa
harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Josephen Bakita,
Parokia ya Igoma Mwanza.
Waliotajwa kuwa ni marafaki wa Sitta ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa
Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.
“Membe, Magufuli na Mwakyembe ni marafiki zangu wa
karibu ambao wana mikono safi na wameniunga mkono siyo wengine walafi,
waongo wanaotutumbukiza katika mikono ya Dowans na Richmond ambao siyo
waadilifu na wazalendo;
“Tuwakatae maana ukiwapa madaraka wataweka
vibaraka wao na nchi itaelekea pabaya na hiyo ndiyo inaweza kuzusha
vurugu kwani ukimnyonya maskini na akiona unamnyonya atataka
kufurukuta...Huo ndiyo mwanzo wa vurugu, nchi haiwezi kutulia kwa hiyo
tuwakatae watu wa namna hiyo,” alisisitiza Sitta.
Hii ni mara ya kwanza kada huyo wa CCM ambaye
amewahi kuliongoza Bunge la Jamhuri wa Muungano kuwataja hadharani
marafiki zake hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika duru za
kisiasa nchini.
Katika harambee hiyo Sitta aliwasilisha zaidi ya
Sh25 milioni ambazo alisema kati ya fedha hizo Sh5 milioni zilitoka kwa
Waziri Membe, Sh5 milioni zingine zilichangiwa na Dk Mwakyembe na Dk
Magufuli huku yeye (Sitta) akichangia Sh5 milioni na pesa zilizobaki
zilichangwa na wabunge wanaowaunga mkono.
Sitta alitaja viongozi wengine ambao
wanashirikiana vizuri na wamemsadia katika harambee hiyo kuwa ni Anna
Kilango, Merry Nagu, William Geleja, Aden Rage, Catherin Majige, James
Lembeli, Mark Mwandosya pamoja na Victor Mwambalaswa ambao wao wote
walimchangia Sh500,000 kila mmoja huku Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii Lazaro Nyalandu akitoa Sh1 milioni.
Awali Sitta aliwataka Watanzania kuthamini kura zao ili wasiangukie katika mikono ya viongozi mafisadi
Na Sheilla Sezzy, Mwananchi
Na Sheilla Sezzy, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment