Romário
(1993), Ronaldo (1996), Rivaldo (1997), Ronaldinho (2003) na Neymar (2013).
Neymar anajiunga ma urithi
mzuri wa washambuliaji wa Brazil unaoundwa na wanaume wanne waliopata mafanikio
makubwa katika miongo kadhaa iliyopita na kupata mafanikio makubwa ndani ya Nou
Camp - sasa ni zamu Neymar da Silva.
Romário na Ronaldo
Romário aliigusa mioyo ya
mashabiki wa Barca kwenye msimu wa 1993-4, wakati alipopewa jina la “cartoon
footballer” kutokana na kuwa uwezo mkubwa mno wa kucheza soka. Aliposajiliwa
alihaidi kufunga mabao 30 ya ligi na akatimiza ahadi yake huku kikosi cha
Cruyff kikishinda ubingwa msimu huo, Romario alirudi Brazil baada ya nusu ya
msimu uliofuatia.
Mara baada ya Romario kuondoka
kinda la miaka 19 - Ronaldo De Lima aliwasili Camp Nou. Alikuwa na nguvu,
mwenye ujuzi na mwenye uchu wa mabao - kwenye msimu wake wa kwanza alifunga
mabao 47 kwenye mechi 51.
Rivaldo na Ronaldinho
Wakati Ronaldo alipohamia
Inter, Rivaldo akaja Camp Nou akitokea Deportivo. Rivaldo akawa nyota wa kikosi
cha Van Gaal kilichoshinda ligi mara mbili. Alifanikiwa kushinda mchezaji wa
dunia mwaka 1999.
Kuwasili kwa Ronaldinho mwaka
2003 kukaleta mageuzi makubwa kwa klabu ya Catalunya na kuleta tabasamu
lilopotea na mashabiki wa Barca. Baada ya ukame wa miaka mitano bila kombe,
aliiongoza Barca kushinda ubingwa wao wa pili wa ulaya jijini Paris na kushinda
uchezaji bora wa ulaya na dunia kwa mara kadhaa.
Evaristo, Giovanni and Anderson
Romário, Ronaldo, Ronaldinho na
Rivaldo wanaweza kuwa ndio washambuliaji wa kibrazil waliopata mafanikio
makubwa zaidi, lakini hawakuwa wa brazil pekee walioleta sura za furaha Camp
Nou. Kwa mfano miaka ya1950s, Evaristo de Macedo alifunga mabao 173 kwenye 219.
Miongo kadhaa baadae mwishoni mwa miaka ya 90, Giovanni Silva na Sony Anderson
pia walileta sura za furaha Catalunya kwa viwango vyao.
Sasa ni zamu ya Neymar - je
atafuata nyayo za magwiji ya Brazil waliomtangulia kucheza Camp Nou na
kuwafunika kabisa kimafanikio? Muda utaongea.
CHANZO:
SHAFII DAUDA
0 comments:
Post a Comment