Thursday, 16 May 2013

GESI MTWARA HOFU YATANDA TENA


o

  • Huduma za vyakula sokoni zitafungwa
  • Huduma za Usafiri kama vile bodaboda , Bajaji na Hiace zisimame
  • Maduka yote yafungwe
  • Ofisi zote zikiwamo za serikali na zisizokuwa za serikali zifungwe.
  • Shughuli zote zisimame mpaka bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini isomwe na mbivu ijulikane na mbichi ijulikane. Hatma ipatikane ya nini kifanyike.

Hii inatokana na sintofahamu pamoja na ahadi ya serikali kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ndipo gesi ingine itolewe kwa matumizi na kuanza kubaini ahadi hizo hazikuwa za kweli na kuanza kuamsha hisia miongoni mwao. Hali hii ikiendelea itasababisha maafa makubwa na hasara kubwa.
Baadhi ya wadadisi wanasema
Wananchi wamejiandaa kwa silaha za jadi, mabomu ya samaki na kuwa na mitandao mingine mikubwa.
 
Nini kinasababisha?
Kubwa linalosababisha ni kiwango cha walionacho na wasionacho kuongezeka
  • Ukosefu wa ajira.
  • Umasikini 
  • Kudorora kwa Elimu.
  • Hali ya kisiasa mkoani Mtwara.
  • Zao la Korosho. 
  • Ahadi na ngonjera zisizotekelezeka za CCM na watu wake.
  • Gesi ni rasilimali ya pekee baada ya Korosho na wananchi wamesema hawakubali gesi yao itoke hivi hivi bila ya kuwafaidisha wao. Kuwepo na " Economic Profit" itakayofaidisha pande zote badala ya "Accounting Profit" itakayoifaidisha Serikali.
  • Kushuka kwa maadili ya Utumishi wa umma.
  • Maeneo mengi yenye rasilimali hayapewi vipaumbele na wanaofaidika nayo ai wenyeji wa maeneo yale. Mfano Geita, Mwadui na maeneo mengine ambayo yamebakia mashimo na wananchi wake kubakia na umasikini mara mbili hatabkabla ya madini kuchimbwa.
  • Watumishi wa Serikali ambao wanajulikana kwa ufisadi lakini serikali haijawachukulia hatua.

Maeneo ambayo ni target:
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • Ikulu ya Serikali
  • Ofisi zote za Serikali
  • Vituo vya Polisi
  • Eneo la ujenzi wa Bomba la gesi
  • Hospitali ya mkoa
  • Ofisi zote za chama Tawala pamoja na viongozi wake
  • Wale wote wanaoshabikia ujenzi wa bomba la gesi liende Dar
  • Mtu yeyote atakayeonekana kama ni msaliti kwenye nia "cause".
  • Nyumba za Wabunge wanaoshabikia bomba la gesi liende Dar.

Kufuatia hali hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa  ,akiongea katika kituo cha PRIDE FM cha Mtwara amewatoa hofu wananchi na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani wao kama Jeshi wamejipanga kuhakikisha usalama wa wananchi unakuwepo na amani inadumishwa.

Endapo serikali itayapuuza madai ya watu wa Mtwara, madhara ambayo yatajitokeza yatakuwa ni mabaya zaidi kwa kipindi kirefu na yatakuwa ni doa lingine katika historia ya Tanzania ukiacha ile ya Udini.

Serikali inatakiwa iyazingatie madai ya watu wa Mtwara pamoja na wananchi wote ili pato la  taifa litolewe kwa usawa na liwe na tija. Isiwe tafsiri ya pato la taifa linatumika kuwafaidisha viongozi.

Serikali iwe na vipaumbele vyenye manufaa kwa wananchi sio mashangingi na kujilundikia mishahara mikubwa na uheshimiwa kwani mwisho wa siku wote tutamezwa na ardhi ya dunia. 

Source:  wovuti

0 comments: