KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama
kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo
mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Kinana alisema hayo leo wakati
akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum,
kilichofanyika kabla ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku
saba mkoani humo.
Kinana alisema, katazo la wanachama
kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla
ya muda halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Chama.
Kinana alisema, kazi
walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti,
Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake
ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu
binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.
Alisema kuwa hivi sasa kazi ya
CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha
miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya
Kikwete.
Alisema moja ya maeneo ambayo
licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana
utekelezaji wa ilani ya CCM, ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini
ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi
ya maendeleo kwa kasi.
Akizungumzia uchaguzi mdogo wa
madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda
uchaguzi huo kwenye kata zote 25 kutokana na mtandao wa chama chake na
imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.
0 comments:
Post a Comment