Friday, May 31, 2013
K'NJARO UPDATE: HOFU YA KIMETA, MIFUGO YAKATAZWA KUINGIZWA ROMBO
SERIKALI imeweka zuio la mifugo kutoka
nchini Kenya na maeneo mengine ya Tanzania kuingizwa wilayani Rombo Mkoani
Kilimanjaro kutokana na hofu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kimeta unaoshambulia
wanyama kama ng’ombe.
Mbali
na zuio hilo, pia serikali imepiga marufuku uchinjaji wa nguruwe ambao
wanadaiwa kulishwa chakula chenye sumu aina ya polad ambao tayari wamesababisha
kifo cha mtu mmoja na wengine wanne kulazwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Rombo, Elinas Parangyo, alisema hivi karibuni kuwa nguruwe wengi
wamekufa na kwamba uchunguzi uliofanywa na wataalamu kutoka jijini Arusha
umegundua sababu ya vifo hivyo ni chakula walichokuwa wakipewa.
“Tulipata
tukio la kimeta ndani ya wilaya na daktari wa mifugo aliyesajiliwa alipiga
karantini ya kutochinja hovyohovyo kama nyama haijapimwa na wataalamu na hiyo
inahusu mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe,” alisema Parangyo.
Uchunguzi
uliofanywa unaonyesha zaidi ya nguruwe 70 wamekufa na kwamba licha ya zuio
hilo, wako baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiwasafirisha kwa kificho na
kwenda kuuzwa katika mikoa mbalimbali nchini.
Mwandishi wetu:Rombo
DIXON BUSAGAGA
0 comments:
Post a Comment