Wednesday, 29 May 2013

MASHOGA WA KWANZA KUOANA LEO, UFARANSA



Ufaransa  itasherehekea  harusi  ya  kwanza  ya  watu  wa  jinsia moja  leo wakati  Vincent Autin  na Bruno  Boileau  kufunga  pingu  za maisha, siku  chache  baada  ya  sheria  ya  ndoa za  watu  wa jinsia  moja  kuidhinishwa kuwa sheria  kamili hali  iliyozusha maandamano makubwa. 
 http://www.washingtonpost.com/rf/image_606w/2010-2019/WashingtonPost/2013/05/18/Foreign/Images/Par7561778-9608.jpg
Autin , mwenye  umri  wa  miaka  40  na Boileau mwenye  umri  wa  miaka  30, watafunga  pingu  za  maisha katika  harusi  itakayofungwa  na  maafisa  wa  serikali  katika  mji wa  kaskazini  wa  Montpellier.

Meya  wa  jiji  hilo  ambaye  anatoka  katika  chama  cha  Kisoshalist atafungisha  ndoa hiyo  katika  jengo  la  halmashauri  ya  jiji, ndoa ambayo  imepangwa  kufanyika  jioni  ya  leo.

Polisi  watakuwepo  kuzunguka  jengo  hilo, baada  ya  maandamano makubwa  kufanyika  siku  ya  Jumapili  na  watu  wanaopinga  ndoa za  aina  hiyo , ambayo  yaligeuka  baadaye kuwa  ya  vurugu. Kiasi ya watu 350 wamekamatwa   kutokana  na ghasia  hizo mjini Paris.

0 comments: