VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA
MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu
wanajihusisha na vitendo vya kishirikina.
Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba
walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza
nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa
sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye
hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana
kumuua kijana huyo hivi karibuni.Kijana
huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga alidai
hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa tangu azikwe
kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za usiku
pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo
wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo.
Wakiwa
kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa
kijiji hicho ambao hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja
na familia zao kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na
kuangushiwa adhabu hizo za kinyama.
Wa kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo
walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla
ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua
nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile.
Baadaye
walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama
kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa kuamini huenda
wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye kurudi Kasaula na
kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia ajuza hao wengine
kisha kuchoma nyumba tatu.
Bibi wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo,
lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga
kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo
kuwachoma na kuwala kwa hasira.
Kamanda
wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo
la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka
waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.
0 comments:
Post a Comment