Monday, 20 May 2013

LORI LA MAFUTA LA PATA AJARI HAPO JANA


 LORI LA MAFUTA LA PATA AJARI HAPO JANA  WANANCHI WAKIMBILIA KUCHOTA MAFUTA
 Picture

 Picha zote via Mbeya Yetu Blog

Picture

Si zaidi ya mara moja na si katika mkoa wa Mbeya tu bali ndani na njeya Tanzania, wameripotiwa watu makumi kwa mamia kupoteza maisha kwa kulipukiwa na moto ambao chanzo chake ni petroli.

Lakini kwa wengine ni ama kumbukumbu hupotea haraka akilini mwao, ama masikio yametiwa nta hawasikii maonyo wala hawaambiliki, au pengine ni taabu zinasukuma mtu kufanya jambo la hatari kwa kuwa anajiona hanacho cha kupoteza.

Pichani ni watu na vidumu vyao, kila mmoja akijitahidi kukinga na kuchota mafuta kutoka kwenye lori  la kampuni la Lake Oili, ambalo limepata ajali katika eneo la mlima Nyoka, Uyole jijini Mbeya.

Source mbeyayetu blog

0 comments: