WALIOKAMATWA VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI IRINGA WAFIKIA 51 , POLISI WAJIPANGA KWA ULINZI MKALI LEO MAHAKAMANI MBUNGE PIA KUUNGANISHWA
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limejipanga kwa ulinzi makali leo jumatatu wakati wa kufikishwa mahakamani watuhumiwa wa vurugu za umachinga mjini Iringa pamoja na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa .
Mbali ya polisi kujipanga kwa ulinzi pia inadaiwa waliokamatwa mbali ya mbunge Msigwa ni watu zaidi ya 51 ambapo badhi yao wamehojiwa na kuachiwa huru huku zipo taarifa kuwa askari wengi zaidi wametoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuweka ulinzi zaidi katika mahakama wakati wa kufikishwa mahakamani mbunge Msigwa na washirika wake katika vurugu hizo.
Mtamdao mbeyagreennews.blogspot.com umeshuhudia ulinzi makali katika kituo cha polisi ambapo askari wa FFU wamezunguka kituo hicho huku ndugu na jamaa wakipigwa stop kufika kituoni hapo kama njia ya kuimarisha ulinzi na usalama zaidi.
0 comments:
Post a Comment