WATOTO pacha wote watano waliozaliwa juzi
katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamefariki dunia.
Pacha
hao walizaliwa salama juzi kwa kufanyiwa upasuaji kutoka kwa mama yao Sophia
Mgaya (28), mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa.
Mganga
Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk. Benedict Ngaiza, alisema kuwa
watoto hao wameishi kwa saa kumi tu na kufariki dunia kutokana na kuzaliwa na
uzito mdogo wa chini ya kilo moja.
Dk.
Ngaiza alibainisha kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, nafasi
yao ya kuishi ni ndogo sana.
Hata
hivyo, hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika
hospitali ya mkoa akiendelea kupata matibabu.
Tukio
la kuzaliwa kwa pacha hao ambalo halijawahi kutokea katika hospitali hiyo
lilitokea juzi majira ya saa 4 asubuhi, huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa
gramu 730, wa pili 810, wa tatu 670, wa nne 820 na wa tano 430.
Watoto
watatu walikuwa wa kiume, wawili wa kike na huu ulikuwa mzao wa pili kwa
mwanamke huyo.
Katika
mzao wa kwanza wa mama huyo ambaye ni mwalimu, alijifungua mtoto mmoja.
0 comments:
Post a Comment