Saturday, 25 May 2013

RAMADHANI MLA WATU APELEKWA HOSPITALI YA WAGONJWA WA AKILI DODOMA

  •  Kijana Ramadhani Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, jana wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Rama ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome aliyeaga dunia tarehe 2 Aprili 2008. 
Picture
Rama akiwa mahakamani, Mei 2013
Picture
Rama na mama yake, Khadija Ally mahakamani, Aprili 2008

0 comments: