WANANCHI TARAFA YA ISIMANI WAMPONGEZA MBUNGE LUKUVI KWA UMEME NA BARABARA YA LAMI
Tanesco wakiendelea kusambaza umeme Tarafa ya Isimani jimboni kwa waziri Lukuvi
...................................................................................................
WANANCHI wa tarafa ya Isimani jimbo la Isimani wilaya ya Iringa
vijijini mkoani Iringa wamempongeza mbunge wa jimbo la Isimani Bw.
Wiliam Lukuvi kwa kuwapigania kupata umeme wa gridi ya Taifa na
ujenzi wa barabara ya lami ya Iringa- Dodoma.
Wananchi hao wametoa pongezi hizo leo katika ukumbi wa Hima
wakati wa semina ya siku moja ya mradi mpya wa kuwasaidia
kuwakopesha n'gombe kupitia mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe
mradi unaofadhiliwa na asasi ya Heifer (HPI)
Kwani wamesema kuwa mbali ya tarafa hiyo ya Isimani na wilaya
nzima ya Iringa vijijini katika Historia ndio ilikuwa ni wilaya
pekee iliyoweza kulisha mkoa wa Iringa kutokana na kuongoza katika
uzalishaji wa mazao ya chakula ila kwa sasa uzalishaji huo
umebaki kuwa historia baada ya eneo hilo kuathiriwa zaidi na
mabadiliko tabia nchi .
Hivyo walisema maisha yao kwa sasa wamekuwa wakitegemea jitihada
mbali mbali ambazo zimeendelea kufanywa na mbunge wao huyo kutokana
na kuendelea kuwapigania kwa kuanzishwa kwa miradi mbali mbali
ukiwemo mradi mkubwa wa umeme ,barabara ya lami na sasa mradi wa
maji ambao utatatua kero ya maji katika tarafa hiyo ya Isimani.
Wananchi hao walisema kuwa moja kati ya changamoto kubwa
zinazowakumba ni pamoja na kukosekana kwa huduma ya maji katika
eneo hilo kutokana na ukame unaokabili eneo hilo ila kwa sasa
suala hilo limekuwa likishughulikiwa na mbunge wao Lukuvi.
Bw Felix Sanga alisema kuwa Kuhusu tatizo la ukame unaoendelea
kuwakumba katika tarafa kuwa suala hilo lina ufumbuzi wake ikiwa
ni pamoja na kujipanga kwa utunzaji wa mazingira kwa wao wenyewe
kuweka utaratibu wa kutunza mazingira yanayowazunguka.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kati ya Iringa- Dodoma
unaoendelea Sanga alisema kuwa mradi huo wa barabara utaweza
kufungua mirango ya kiuchumi kwa wananchi wa tarafa hiyo ya Isimani
na kupongeza jitihada za mbunge na jinsi anavyoendelea kupigania
maendeleo ya wananchi wake.
Kwa upande wake mtaalam kutoka asasi hiyo ya Kimataifa ya Heifer
Interinational Dr Emmanuel Sokonde alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni
maandalizi ya kuandika andika maalum kwa ajili ya kushawishi asasi hiyo
kusaidia miradi ya kiuchumi ukiwemo mradi wa ufugaji wa ng'ombe.
Hivyo alisema kuwa lengo la asasi hiyo ni kuwakomboa watanzania na
kuwatafutia miradi yenye kuwakwamua kiuchumi zaidi na kuwa iwapo
watafanikiwa mradi huo kufika eneo hilo basi itakuwa ni faida kwa wananchi
wa tarafa hiyo.
0 comments:
Post a Comment