(Mchunguzi wetu kutoka Dar):
Majira ya saa 9:00 alasiri, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni
jijini Dar es Salaam, kijana mmoja (poichani) alikurupushwa kwa kupigiwa
kelele za 'mwizi' na mtu aliyedai kutapeliwa naye. Wananchi walianza
kumkimbiza hadi walipogotea maeneo ya Vijana, Kinondoni baada ya
mtuhumiwa kujikwaa na kuanguka. Baada ya adayedaiwa kutapeliwa
kuwafahamisha mkasa wa kutapeliwa shilingi 350,000/-, wananchi
walimpekua
mtuhumiwa
na kukutwa na makaratasi yaliyokatwa na kufungwa kwa noti bandia za
shilingi elfu kumi, vitambulisho vya watu mbalimbali kama vile leseni,
picha za pasipoti, barua za serikali za mitaa za jijini Dar es Salaam
n.k. Alipoulizwa kuwa vitu hivyo vya watu na nyaraka za serikali ni vya
nini au alivipataje, jamaa huyo alijitetea kuwa ana mtu anayeshirikiana
naye katika shughuli hiyo. Salama yake ya kutokuuawa na kuachwa akiwa
katika hali mbaya, ilikuja baada ya madereva wa taxi wa eneo hilo kusema
hawataki kuachiwa ushahidi wa kuchoma moto mtu huyo katika eneo lao.
0 comments:
Post a Comment